• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Tyson Fury asema pambano lake la tatu na Deontay Wilder litakuwa gumu na lenye ushindani mkubwa

    (GMT+08:00) 2020-05-27 08:33:43

    Bingwa wa uzito wa juu Duniani Tyson Fury amesema kuwa mpambano wake wa tatu dhidi ya Deontay Wilder utakuwa ni mgumu na wenye ushindani mkubwa, kutokana na kiu ya kisasa aliyokuwa nayo mpinzani wake baada ya kumchakaza katika pambano lililopita. Fury alimpiga Wilder katika pambano la uzito wa juu wa Dunia (WBC), Februari mwaka huu, ambapo hadi kufikia raundi ya saba tayari Wilder alishaanguka chini mara mbili, baada ya pambano lao la kwanza kumalizika kwa sare. Kwasasa Wilder anajiandaa kwa ajili ya pambano la tatu la marudiano akiamini kuwa litakuwa na ugumu wa aina yake. Pambano hilo la tatu la marudiano kati ya mabondia hao wawili, linatazamiwa kwenda kupiganwa nje ya Marekani na Uingereza kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya Corona. Fury ambaye anashika nafasi ya kwanza ya ubora kwa mabondia wa uzito wa juu, ameshinda jumla ya mapambano 30, huku 21 yakiwa ni kwa KO na kutoka sare pambano moja, wakati akiwa hajapoteza pambano hata moja, katika jumla ya mapambano 31 aliyocheza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako