• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aliyekuwa mkuu wa Baraza la Kutunga Sheria la Hong Kong asema utungaji sheria ya usalama wa taifa kwa Hong Kong ni muhimu

    (GMT+08:00) 2020-05-27 09:59:00
    Aliyekuwa mkuu wa Baraza la Kutunga Sheria la Hong Kong Bi. Rita Fan Hsu Lai-tai amesema mchakato wa kujadili hoja ya kutunga sheria ya usalama wa taifa kwa Hong Kong katika mkutano wa Bunge la Umma la China umekuja kwa wakati, ni muhimu na ni wa lazima.

    Bi. Rita Fan Hsu Lai-tai amesema watu wenye msimamo mkali wameleta vurugu mara kwa mara, wakijaribu kuivuruga kabisa Hong Kong, hivyo ni lazima kuchukua hatua ya kuondoa mapungufu ya kisheria ya Hong Kong katika kulinda usalama wa taifa dhidi ya wale wanaopinga serikali kuu ya China na kuleta fujo Hong Kong. Ameongeza kuwa kutunga sheria hiyo kutaweza kuhakikisha "Nchi Moja, Mifumo Miwili" kutekelezwa vizuri na pia ni msingi muhimu wa kulinda utulivu na ustawi wa Hong Kong.

    Habari nyingine zinasema hadi kufikia usiku wa Jumanne, wakazi wa Hong Kong zaidi ya milioni 1.1 walisaini barua ya kuunga mkono utungaji sheria ya usalama wa taifa kwa Hongkong. Shughuli hiyo ya kusaini barua ilianza Jumapili na shirika lililoundwa hivi karibuni na maelfu ya watu na makundi kutoka sekta mbalimbali katika jamii ya Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako