• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kocha wa Yanga awapa ushauri TFF

    (GMT+08:00) 2020-05-27 15:46:51

    Kocha Mkuu wa timu ya Yanga nchini Tanzania Luc Eymael, amefunguka kwamba licha ya Serikali kuruhusu michezo lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wanatakiwa kutoa muda kwa ajili ya timu kupata nafasi ya kufanya mazoezi ya pamoja. Kocha huyo amesema hawawezi kurejea na kuanza kucheza ligi Juni Mosi ambapo michezo imeruhusiwa kwa sababu wachezaji hawakuwa pamoja kwa muda mrefu, hivyo wanahitaji tena muda mfupi wa maandalizi kabla ya ligi kuanza. Serikali imeruhusu kuendelea kwa shughuli za kimichezo nchini, huku michezo yote ya Ligi Kuu iliyobakia imepangwa kuchezwa kwenye viwanja vya Dar Uhuru, Taifa na Azam Complex.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako