• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong ni matumaini ya kulistawisha eneo hilo

    (GMT+08:00) 2020-05-27 20:00:01

    Mkutano wa tatu wa Bunge la 13 la Umma la China umekagua na kujadili mswada wa azimio la kujenga na kukamilisha mfumo wa sheria na utaratibu wa utekelezaji wa kulinda usalama wa taifa wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, hatua inayoungwa mkono na jamii ya Hong Kong.

    Jamii mbalimbali za Hong Kong zimeanzisha kampeni ya kuunga mkono utungaji wa sheria hiyo kupitia kukusanya saini kwenye mtandao wa Internet, na hadi tarehe 26, saini milioni 1.1 zimekusanywa ndani ya siku tatu. Watu wameona kwa uwazi kuwa sheria ya usalama wa taifa ya Hong Kong ni matumaini ya kulistawisha eneo hilo.

    Kutokana na uchochezi wa baadhi ya wanasiasa wa nchi za magharibi na Marekani, watu wachache wanaojaribu kuitengenisha Hong Kong na China na watu wanaovuruga utulivu wa mkoa huo wanaendelea kufanya vitendo vinavyovuruga na kuathiria vibaya maisha ya wakazi wa eneo hilo na utulivu wa jamii.

    Kutungwa kwa sheria hiyo kunaendana na maslahi ya msingi ya taifa na Hong Kong, pia kutanufaisha haki halali na uhuru wa wakazi wa eneo hilo na kutambuliwa na jamii ya Hong Kong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako