• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Ziwa Nyasa kuvutia watalii wengi zaidi

    (GMT+08:00) 2020-05-28 19:55:57
    Uwekezaji kwenye Fukwe za Ziwa Nyasa zilizopo wilayani Kyela katika Mkoa wa Mbeya, unadaiwa kuwa unaweza kuongeza idadi ya watalii katika ukanda wa Nyanda za Juu Kusini na kuinua uchumi wa Taifa endapo kutakuwa na wawekezaji wa kutosha.

    Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, wakati akikagua miundombinu ya barabara kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa ambapo aliwakaribisha watu wenye uwezo kuwekeza kwenye fukwe za ziwa hilo.

    Alisema Wilaya ya Kyela ina fukwe nzuri mwambao mwa Ziwa Nyasa na, kwamba hata kina cha ziwa sio kirefu sana, hii ni fursa sasa kwa wadau kutumia fursa ya kujenga hoteli na miundombinu mingine ambayo itavutia watu kutembelea.

    Aidha, Chalamila alisema uwapo wa meli mbili mpya za mizigo na moja ya abiria ambazo zimejengwa na Serikali ya Tanzania ndani ya Ziwa Nyasa pia ni kichocheo kingine cha biashara inayoweza kuinua uchumi kwa Watanzania kupitia Ziwa Nyasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako