• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: EPL kurejea tena Juni 17

    (GMT+08:00) 2020-05-29 08:36:24

    Kampeni za Ligi Kuu ya Uinegreza (EPL) sasa zitarejea tena Juni 17, 2020, kwa mechi mbili zitakazokutanisha Aston Villa na Sheffield United kisha Manchester City na Arsenal. Mechi hizo ni zile zilizokuwa zimesalia kwa vikosi hivyo kucheza ili kufikia idadi ya michuano 29 ambayo wapinzani wote wengine 16 walikuwa wamepiga hadi kipute hicho kiliposimamishwa kwa muda kutokana na janga la corona mwanzoni mwa Machi 2020. Mechi zote za raundi nzima ya 30 zimepangwa kuchezwa kati ya Ijumaa ya Juni 19 na Jumapili ya Juni 21, 2020. Hadi kampeni za EPL zilipoahirishwa, zilikuwa zimesalia jumla ya mechi 92 za kutandazwa msimu huu. Mechi zote zilizosalia zitasakatwa ndani ya viwanja vitupu bila kuwepo mashabiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako