• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kipenga cha kuashiria kurejelewa kwa Serie A kupulizwa rasmi Juni 20

    (GMT+08:00) 2020-05-29 15:55:18

    Waziri wa Michezo nchini Italia, Vincenzo Spadafora ametangaza kuwa, kivumbi cha Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kitaanza tena Juni 20, 2020. Ligi hiyo iliahirishwa Machi 9, 2020, zikiwa zimesalia raundi 12 za mechi za kusakatwa kabla ya msimu huu kumalizika rasmi. Hadi kufikia wakati huo, mabingwa watetezi Juventus walikuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo kwa point 63, moja zaidi kuliko Lazio ambao wanashikilia nafasi ya pili. Wachezaji wa Serie A walianza mazoezi ya kila mmoja kivyake mwanzoni mwa mwezi huu kabla ya kuruhusiwa kushiriki mazoezi katika makundi madogo ya watu watano mwanzoni mwa wiki hii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako