• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Asilimia 75 ya kampuni huenda zikafungwa Juni – CBK

    (GMT+08:00) 2020-05-29 21:14:24
    Hali ya uchumi nchini Kenya inazidi kudorora kutokana na makali ya janga la Covid-19, huku serikali ikionya huenda Wakenya wengi zaidi wakapoteza ajira kufikia mwishoni mwa mwezi Juni.

    Kwa muhibu Gavana wa Benki Kuu ya Kenya (CBK) Dkt Patrick Njoroge, huenda asilimia 75 ya kampuni ndogo na zile za wastani zikalazimika kufunga biashara kutokana na ukosefu wa fedha mwezi ujao.

    Dkt Njoroge alisema kampuni hizo zinafaa kulindwa dhidi ya hatari ya kuporomoka kwani zinachangia pakubwa kwa kuinua viwango vya ajira pamoja na utajiri wa nchi. Wakati huo huo, hoteli ya kifahari ambayo imekuwa ikihudumu humu nchini kwa miaka 116, Fairmont Norfolk, ilifunga hoteli zake na kuwatimua wafanyakazi wote.

    Meneja wa hoteli hizo humu nchini Bw Mehdi Morad, alisema uamuzi huo ulifikiwa kutokana na hali kwamba haijulikani ni lini virusi vya corona vitadhibitiwa na watu kuruhusiwa kuendelea na biashara zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako