• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutoka Garner hadi Floyd, mauaji ya ubaguzi wa rangi yaendelea kutokea Marekani

    (GMT+08:00) 2020-05-30 18:08:26

    Idadi ya wamarekani wanaouawa kwa kushindwa kupumua inaonekana sio Goegre Floyd peke yake aliyeuawa na polisi kwa kukandamizwa chini. Maandamano ya sasa na hasira inayoonekana karibu katika nchi nzima ya Marekani, yanatokana na watu kutosahau kifo cha Eric Garner cha mwaka 2014. Vurugu za Ferguson, mauaji makubwa ya El Paso Texas, na mwanamke mwenye asili ya Afrika aliyeuawa nyumbani kwake mwaka huu. Maneno ya mwisho aliyosema mtu aliyekuwa hivi karibuni yanafanana kabisa na maneno aliyosema Eric Garger kabla ya kifo chake baada ya kukabwa, "siwezi kupumua" Lakini cha ajabu ni kuwa Daniel Pantaleo, polisi aliyemuua Eric Garder alilindwa na mahakama na hakuhukumiwa.

    Tarehe 9 Agosti 2014, mwezi mmoja baada ya kuuawa kwa Bw. Gardner, tukio lingine lilitokea katika mji wa Ferguson katika jimbo la Missouri, ambapo kijana mwenye umri wa miaka 18 Michael Brown, alipigwa risasi na kuuawa na polisi mzungu Darren Wilson baada ya kumkamata shingoni kupitia dirisha la gari lake na kumtishia. Kwenye tukio hili pia mahakama iliamua kutomchukulia hatua Daarren Wilson.

    Matukio mengine ya mauaji kama hayo yaliripotiwa katika miji mingine ya Marekani ikiwa ni pamoja na Baltimore, Chicago, Minneapolis, Oakland nk., na kufanya kuwa na wimbi la maandamano katika nchi nzima, kwa jina la harakati ya "black lives matter" yaani maisha ya watu weusi pia ni muhimu.

    Mauaji haya yanaonyesha mfumo wa muda mrefu wa kukosekana haki nchini Marekani. Katika miaka ya hivi karibuni tangu rais Trump aingie madarakani, ameandaa orodha ndefu ya kauli zinazowahusu wamarekani wenye asili ya Afrika, Wamexico, Wasia, Wenye asili ya Hispania, Wamarekani wazawa, waislamu, wayahudi na wahamiaji kwa ujumla, hata watu wenye ulemavu. Kwa yeye kutoa hukumu ya kifo kwa watu weusi kwenye kauli aliyotoa kuwa "uporaji ukianza, ufyatuaji risasi unaanza" inaonyesha kuwa mfumo wa muda mrefu wa kukosekana kwa haki nchini Marekani umefika kwenye kiwango cha juu.

    Mwezi Agosti mwaka 2019, kijana akiwa na bunduki aina ya gobole alifyatua risasi kwenye supamaketi ya Walmart El Paso Texas, na kuwaua watu 20 na kuwajeruhi wengine 26, siku sita tu tangu mtu mwenye silaha kuwaua watu watatu kwenye tamasha la chakula Kaskazini mwa California. Wizara ya Sheria ya Marekani ilisema mauaji hayo yalichochewa na chuki dhidi ya kundi fulani la watu. Muuaji mzuri aliweka ujumbe kwenye mtandao wa kijamii akisema "shambulizi hili ni jibu kwa uvamizi wa wa-hispanic kwenye jimbo la Texas". Mapema mwaka huu mhudumu wa afya alipigwa risasi nane nyumbani kwake, wakati polisi wakimsaka mtu ambaye haishi kwenye nyumba yake.

    Takwimu zilizokusanywa na gazeti la Washington Post, zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2015 na 2019 watu wenye asili ya Afrika walikuwa wahanga wa matumizi ya mabavu ya polisi. Licha ya kuwa polisi wamejitetea kuwa kuna sababu za kimsingi za wao kufanya hivyo, lakini swali ni kwanini waliowachache ndio wanalengwa zaidi? Lakini bila kujali ni sababu gani, ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa makazi, hali ya kiuchumi, kutokuwepo kwa usawa wa shule, umwamba wa wazungu, kufumbua macho ubaguzi, kuweka vikwazo watu kupiga kura, ubaguzi kwenye ajira n.k vifanywa hali ya ubaguzi wakati wa serikali ya Trump kuwa mbaya zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako