• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asisitiza umuhimu wa Kanuni ya Mambo ya Kiraia katika kulinda vizuri haki halali na maslahi ya watu

    (GMT+08:00) 2020-05-30 18:09:59

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza utambuzi kamili wa umuhimu wa utoaji na utekelezaji wa Kanuni ya Mambo ya Kiraia iliyoidhinishwa hivi karibuni na kulinda vizuri zaidi haki halali na maslahi ya watu, kuendana na sheria.

    Rais Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC alitoa kauli hizo Ijumaa alipoendesha mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC kuhusu utekelezaji mzuri wa Kanuni ya Mambo ya Kiraia.

    Rais Xi amekitaka Chama kizima kutekeleza ipasavyo Kanuni hiyo ili kukuza utawala bora wa taifa na ujenzi wa nchi inayofuata mfumo wa ujamaa kwa kufuata sheria na kulinda haki na maslahi ya watu.

    Akielezea kuwa Kanuni ya Mambo ya Kiraia ni sheria ya kwanza kutumia neno "kanuni" tangu Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa mwaka 1949, rais Xi amesema hii imeonesha mafanikio makubwa ya nchi hiyo katika kuendeleza utawala wa kisheria wa kijamaa katika zama mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako