• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yaruhusu kufungua sekta ya utalii taratibu licha ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-05-31 18:41:05

    Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kufungua sekta ya utalii hatua kwa hatua na kulegeza vizuizi vya COVID-19 kuanzia kesho tarehe mosi, Juni.

    Waziri wa utalii Mmamoloko Kubayi-Ngubane amesema kwa jinsi janga la virusi vya Corona linavyotarajiwa kuendelea, sekta ya utalii itafunguliwa kwanza kwa soko la ndani ya nchi, ikifuatwa na utalii wa kikanda na wa kimataifa mwaka ujao.

    Tarehe 24, Mei, rais Cyril Ramaphosa ametangaza kuwa zuio kwa nchi nzima litapunguziwa ngazi kutoka ya 4 hadi 3 kuanzia kesho, hali ambayo itaruhusu viwanda vingi kuanza uzalishaji na mamilioni ya watu kurudi kazini pamoja na kufunguliwa tena kwa shule.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako