• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China nchini Marekani aeleza sababu na kujibu wasiwasi wa watu juu ya utungaji sheria ya usalama wa taifa kwa Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-05-31 18:45:50

    Balozi wa China nchini Marekani Cui Tiankai amesema sheria ya kulinda usalama wa taifa kwa Hong Kong itahakikisha kuwa sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" sio tu itatekelezwa ipasavyo, bali pia kwa muda mrefu, kwani Hong Kong haitakuwa na maendeleo na ustawi wa kudumu kama usalama wa taifa haukuwepo.

    Balozi Cui amesema hayo katika makala yake iliyochapishwa kwenye tovuti ya Bloomberg Opinion jana tarehe 30 juu ya uamuzi wa Bunge la Umma la China kuanzisha na kuboresha mfumo wa kisheria na taratibu za utekelezaji wake kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa katika Eneo lenye Utawala Maalum la Hong Kong.

    Balozi Cui amesema kwa kutegemea kutokuwepo kwa sheria ya usalama wa taifa katika Hong Kong, baadhi ya watu wa eneo hilo wamechochea vurugu na kutaka "kujitenga" kwa Hong Kong, wakivuka mstari mkuu wa serikali kuu. Wakati huohuo, nchi za nje zimezidi kuingilia kati masuala ya Hong Kong bila kujali chochote. Mambo hayo yamesababisha Hong Kong iingie kwenye ghasia na usalama wa taifa la China kuwa hatarini.

    Balozi Cui amesema hii ndio sababu ya serikali kuu kuamua kuchukua hatua. Kwa mujibu wa Ibara ya 23 ya Sheria ya Msingi, Eneo lenye Utawala Maalumu la Hong Kong limepewa idhini ya kutunga sheria yenyewe kulinda usalama wa taifa. Lakini sheria kama hizo hazikutungwa katika miaka 23 iliyopita tangu Hong Kong irudi China, kutokana na makundi ya upinzani kujaribu kwa njia zote kuzuia. Hali hii imelilazimisha Bunge la Umma la China kutunga sheria husika, uamuzi ambao umepokelewa na kuungwa mkono na watu wa China wakiwemo wa Hong Kong, na wengi wao wameamini kuwa zingetungwa tangu siku za nyuma.

    Juu ya mashaka ya watu kama China ina madaraka ya kuchukua hatua hiyo, balozi Cui amesema katika nchi zote, iwe serikali ya jamhuri ama serikali ya shirikisho, ni serikali kuu ndio ina madaraka kwa mujibu wa sheria ya kuamua masuala yanayohusu usalama wa kitaifa. Hali kadhalika, serikali kuu ya China ina wajibu wa kimsingi na wa mwisho wa kulinda usalama wa taifa, na Bunge la Umma la China ni chombo cha ngazi ya juu kabisa cha kutunga sheria nchini China.

    Kuhusu wasiwasi wa watu kuwa kama sheria hiyo itaharibu sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili", balozi Cui amesema uamuzi huo wa Bunge la Umma la China umedhihirisha kuwa kanuni za "Nchi Moja, Mifumo Miwili", "watu wa Hong Kong waongoza Hong Kong" na "kiwango cha juu cha kujiongoza zitatekelezwa ipasavyo na kwa usahihi. Amesema usalama wa taifa ni msingi wa "Nchi Moja, Mifumo Miwili", nguvu yake inaweza kukuzwa katika jamii yenye usalama na utulivu.

    Balozi amesisitiza kuwa sheria hiyo inalenga vitendo vinavyoharibu usalama wa taifa la China kama vile kutenganisha nchi, kupindua serikali, kufanya shughuli za kigaidi na nchi za nje kuingilia kati masuala ya Hong Kong, kwa hivyo watu wasiojihusisha na vitendo hivyo hawana haja ya kuwa na wasiwasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako