• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa masuala ya China aeleza jinsi ya kuwa na hoja zenye mantiki juu ya sheria ya usalama wa taifa iliyopendekezwa na China

    (GMT+08:00) 2020-05-31 19:00:13

    Hivi karibuni China ilipendekeza Sheria ya Usalama wa Taifa, ikizingatia zaidi Hong Kong na kupokelewa kwa matumaini makubwa na Bunge la Umma la China NPC. China imesema sheria hiyo inaimarisha sera ya "nchi moja, mifumo miwili" kwa kupunguza ghasia za waandamaji na wahuni. Hata hivyo sheria hiyo imekuwa ikikosolewa na baadhi ya watu wakidai kwamba inadhoofisha sera hiyo kwa kuruhusu uingiliaji wa nguvu wa jeshi la usalama wa taifa.

    Kufuatia ukosoaji huo mtaalamu wa masuala ya China kutoka New York Marekani Robert Lawrence Kuhn ameelezea jinsi ya kuwa na hoja zenye mantiki juu ya sheria ya usalama wa taifa iliyopendekezwa na China. Amesema ukosoaji huo umeweka kipaumbele kwenye mifumo miwili wakati China imeweka kipaumbele kwenye nchi moja. Katibu mkuu wa NPC Wang Chen ameelezea kilichochochea sheria hiyo ni kwa sababu ya wale wanaoipinga China, na kuvuruga utulivu wa Hong Kong kwa kuhamasisha kwa uwazi "uhuru wa Hong Kong", na kusisitiza kuwa lazima kuwepo na hatua kali zilizo chini ya sheria ili kuzuia, kusitisha na kuwaadhibu.

    Hata hivyo Bw. Kuhn amesema naibu waziri mkuu Han Zhang anaonekana kusawazisha mambo, na kuelezea ukomo wa Sheria kwa kuhakikisha kwamba italenga kundi dogo tu la watu ili kuzuia vurugu za waandamanaji wanaopinga serikali, ikiwa na lengo la kuwasaidia, na sio kuwaumiza raia wa kawaida.

    Ni jinsi gani ya kuelewa mantiki ya China? Kwa muktadha huu, umuhimu wa mwaka huu wa 2020, unaonekana kwenye "jamii yenye maisha bora", ambayo ni sehemu ya kwanza ya Rais Xi Jinping anayoita "Uhuishaji Mkubwa wa Taifa la China". Kuna nguzo mbili zinazosaidia Uhuishaji Mkubwa, moja ni maendeleo ya uchumi na ya pili ni mamlaka ya taifa kama sehemu muhimu ya ufahari wa taifa. Vurugu za Hong Kong zimekuwa kidonda kwenye nguzo hii, na uongozi wa China umedhamiria kukiponya kidonda hiki.

    Bw. Kuhn ameendelea kufafanua kuwa serikali kuu inataka kukuza Hong Kong, na sio kuidhibiti. Hivyo, serikali kuu itaiunga mkono Hong Kong kadiri iwezavyo, lakini amesititiza kuwa kuna mistari mitatu myekundu ambayo haipaswi kuvukwa. Kwanza ni harakati za Hong Kong za kujitenga, kutumia Hong Kong kudhoofisha mfumo wa siasa unaongozwa na bara, na vurugu zisizoisha ambazo zitatishia uchumi wa Hong Kong. Hivyo amesema sheria hii mpya itapunguza hali ya kutokuwa na uhakika kwa kuzuia hali ya kutokuwa na utulivu. Ameshauri kuwa ili sheria hii ifanye kazi vizuri, ni lazima isiingile kati uhuru wa Hong Kong na uhuru wa vyombo vya habari. Na kusema kuna udhaifu duniani, hivyo hata tatizo dogo linaweza kuvuruga kila kitu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako