• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Yanga yasaini mkataba na La Liga kwa ajili ya kuwaongoza katika mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wake

    (GMT+08:00) 2020-06-01 08:53:52

    Klabu ya Yanga ya Tanzania jana ilisaini mkataba na Bodi ya Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) kwa ajili ya kuwaongoza katika mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wake. Inaelezwa kwamba mkataba huo utaifanya Yanga iwe kama Seville iliyowahi kwenda Tanzania na kucheza na Simba na kushinda mechi hiyo ya kirafiki kwa mabao 5-4. Mkataba huo utasainiwa ukiishirikisha pia kampuni ya GSM ambayo ndio itakayogharamia mchakato huo. Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema moja kati ya azma za mwenyekiti Dk Mshindo Msolla tangu anachukua nafasi, shabaha yake ilikuwa ni kufanya mabadiliko ya kuitoa klabu ilipo katika uendeshaji tegemezi kwenda kuwa ya kujitegemea. Amebainisha kuwa sio GSM wanaofanya mabadiliko bali mabadiliko yatafanywa na Yanga. Nugaz alisema uamuzi wa kuishirikisha La Liga umetokana na uzoefu walionao kutokana na uendeshaji na mafanikio ya soka ya Hispania. Naye Katibu Mkuu wa Yanga, David Ruhago alisema ni mwanzo wa kuipeleka klabu hiyo kwenye mafanikio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako