• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mechi Tanzania kupigwa kama kawaida nyumbani na ugenini wakiwepo mashabiki

    (GMT+08:00) 2020-06-01 08:54:38

    Sasa ni rasmi kwamba mechi zote Tanzania zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini bila kuwepo vituo kama ambavyo ilielekezwa awali huku mashabiki wakiruhusiwa kuingia viwanjani. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Hassan Abass, amesema kuwa suala hilo limezingatia maoni ya Wizara ya Afya pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya michezo. Vituo ambavyo vilipangwa awali ilikuwa ni kwa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho kituo cha Dar es Salaam na zile za Ligi Daraja la Kwanza na la Pili zingechezwa Mwanza. Hii ilikuwa ni kutokana na kuchukua tahadhari dhidi ya janga la Virusi vya Corona ambalo linaivuruga dunia. Ligi inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 13.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako