• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe kuimarisha hatua za usalama kwenye vituo vya karantini mipakani

    (GMT+08:00) 2020-06-01 09:04:04

    Waziri wa habari, uenezi na utangazaji wa Zimbabwe Bibi Monica Mutsvangwa, amesema Zimbabwe itaimarisha hatua za usalama kwenye vituo vya karantini nchini kote ili kuzuia kutoroka kwa watu walioko kwenye karantini.

    Bibi Mutsvangwa amesema serikali ya Zimbabwe itaimarisha hatua za usalama, hasa kwenye maeneo ya mpakani ili kuzuia kuenea kwa COVID-19.

    Bibi Mutsvangwa pia amesema serikali inafanya juhudi kutumia droni ili kuongeza hatua za usalama kwenye maeneo ya mpakani. Hivi karibuni zaidi ya watu 118 wametoroka kutoka kwenye vituo vya karantini nchini Zimbabwe, na kuzua hofu ya mlipuko wa COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako