• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakabidhi jengo jipya la taasisi ya Confucious kwa Chuo Kikuu cha Nairobi

    (GMT+08:00) 2020-06-01 09:28:02

     

    Jengo jipya la Taasisi ya mafunzo ya lugha ya kichina katika barabara ya Aboretum jijini Nairobi limekabidhiwa rasmi kwa Chuo Kikuu cha Nairobi.

    Hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliongozwa na Balozi wa China nchini Kenya Wu Peng na Waziri wa Elimu Kenya,Profesa George Magoha.

    Jengo hilo lilijengwa na serikali ya China kwa gharama ya Ksh1.4bn.

    Jengo hili jipya la taasisi ya mafunzo ya lugha ya Kichina ya Confucious limejengwa na serikali ya China kwa gharama ya Ksh1.4 bilioni.Jengo hili lina madarasa,kumbi za mikutano,mabweni ,ofisi za wafanyakazi na maktaba na ofsi za utafiti wa lugha ya kichina.

    Waziri wa Elimu Profesa George Magoha alisema kuwa tangu mwaka 2003 ,zaidi ya wakenya 17,000 wamefunzwa lugha ya kichina.

    Alisema miongoni mwao ni wafanyakazi wa serikali walio katika sekta ya usafiri wa anga na utalii,biashara na viwanda,maafisa wa vyuo vikuu na wanafunzi,miongoni mwa wengine.

    Aidha aliutaja mradi wa reli ya kisasa ya SGR kama mradi mkuu ambao umeboresha uhusiano kati ya Nairobi na Beijing.

    Profesa Magoha alitoa changamoto kwa Naibu Kansela wa Chuo Kikuu cha Nairobi kulitumia jengo hilo kikamilifu na kuongeza idadi ya idadi ya wanafunzi wanaotaka kujifunza lugha ya kichina na utamaduni.

    Magoha alidokeza kuwa lugha ya kichina huenda ikawa mojawapo ya lugha zinazofunzwa katika shule za msingi.

    "Mtaala wenye msingi wa uwezo ni muhimu na miongoni mwa mahitaji yake ni mafunzo ya lugha kuanzia gredi ya 4 katika shule za msingi.Hakuna sababu kwa nini moja ya lugha hizo isiwe ni kichina"

    Profesa Magoha alisema ujenzi wa jengo hilo la taasisi ya Confucious katika Chuo Kikuu cha Nairobi utatoa fursa kwa walimu wengi zaidi kujifunza lugha ya kichina wanapojitayarisha kuijumuisha lugha hiyo katika mtaala mpya wa elimu.

    "Kwa kuwa tuko na shule za msingi takriban 30,000 ,hii ni fursa ya kuwapatia mafunzo walimu ambao watawafunza wanafunzi lugha ya kichina ,na pia kuihimiza serikali ya watu wa China kushirikiana na sisi katika mchakato huu na kuhakikisha watoto ambao wana ari ya kuwa wataalamu wa lugha ya kichina wanaanza..hiyo ni faida nyingine"

    Balozi wa China nchini Kenya Wu Peng alisema kuwa serikali ya China inapatia umuhimu mkubwa mabadilishano ya elimu kati ya Kenya na China.

    Kwa maana hiyo,kumekuwa na wanafunzi zaidi ya 1,000 wanaopewa ufadhili wa masomo na serikali ya China.Hii imewezesha wanafunzi wengi kuendeleza masomo yao nchini China.

    Balozi Peng aliahidi kuendelea kuisaidia taasisi ya Confucious kwa kujenga maktaba nyingine mpya ya kisasa itakayokuwa na vitabu,kompyuta na vifaa vingine vinavyohitajika kwa masomo.

    Alisema hiyo itawasaidia watu kuelewa vizuri utamaduni wa China.

    Aliongeza kuwa ujenzi wa jengo ambalo amelikabidhi kwa Chuo Kikuu cha Kenyatta unaenda mbele zaidi katika kuimarisha zaidi uhusiano kati ya Kenya na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako