• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maandamano kutokana na kifo cha George Floyd yaendelea katika miji mbalimbali nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2020-06-01 09:58:11

    Maandamano kutokana na kifo cha George Floyd yanaendelea katika miji mbalimbali nchini Marekani na kusababisha vurugu kubwa nchini humo.

    Shirika la habari la Marekani NBC limeripoti kuwa, waandamanaji wengine 300 huko New York walikamatwa usiku wa Jumamosi, katika siku ya tatu ya maandamano, na waandamanaji zaidi ya 100 walikamatwa usiku huo huko Houston.

    Gavana wa Jimbo la Texas Bw. Greg Abbott ametangaza hali ya maafa kufuatia maandamano ya kimabavu kusambaa kwenye miji mbalimbali jimboni humo. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya gavana huyo inasema, hatua hiyo inamruhusu Bw. Abbott kutuma maofisa wa kutekeleza sheria kuitikia matishio yanayooendelea.

    Mbali na hayo mji wa Los Angeles umetangaza amri nyingine ya kutotoka nje kuanzia saa mbili jioni ya Jumapili hadi saa kumi na moja alfajiri ya Jumatatu ili kujiandaa kwa ajili ya maandamano yatakayofanyika kutokana na kifo cha George Floyd.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako