• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kahata arejea kambini Simba SC

    (GMT+08:00) 2020-06-01 15:40:46

    Kiungo matata wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Francis Kahata aliwasili jijini Dar es Salaam, Tanzania kuungana na wanasoka wenzake wa kikosi cha Simba SC. Wachezaji wa Simba walianza upya mazoezi ya pamoja mapema wiki hii baada ya serikali kutangaza mipango ya kuanza tena kwa Ligi Kuu Juni 13, 2020. Kahata amesema barua kutoka kwa vinara wa Simba SC ndiyo iliyomwezesha kuvuka vizuizi vya maafisa wa usalama barabarani kabla ya kuingia Tanzania licha ya amri inayozuia safari za abiria kwenye mipaka ya Kenya na Tanzania. Simba ambao wanaongoza kilele cha msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania walikuwa wamesalia na jumla ya mechi 10 muhula huu kabla ya ligi kusimamishwa Aprili kutokana na janga la corona. Kahata anatarajiwa kuwa nguzo muhimu kambini mwa Simba ambao wanawania jumla ya mataji mawili kwa mpigo katika kampeni za msimu huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako