• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sehemu zilizoathirika zaidi na virusi vya Corona nchini Afrika Kusini kuwekwa kwenye kiwango cha juu zaidi cha tahadhari

    (GMT+08:00) 2020-06-01 17:02:36

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema sehemu zilizoathirika zaidi na maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo zinaweza kuwekwa kwenye kiwango cha juu zaidi cha tahadhari kama hatua maalum za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo zikishindwa.

    Rais Ramaphosa amesema serikali yake ilichukua njia tofauti kwenye maeneo yenye maambukizi ya kiwango cha juu na maeneo yenye maambukizi ya chini, ambayo yanahitaji kuwa na umakini na usimamizi wa hali ya juu.

    Rais Rmaphosa alisema hayo jana, ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kupunguza kiwango cha tahadhari kutoka nne hadi tatu kwa Afrika Kusini, ambapo watu milioni 8 wataruhusiwa kurudi kazini kutokana na sekta nyingi za kiuchumi kufunguliwa tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako