• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto wa Kibera nchini Kenya warekodi maisha ya kila siku chini ya mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-01 17:09:39
    Kibera ni eneo kubwa zaidi la makazi duni nchini Kenya, ambapo malaki ya watu wanaishi kwenye eneo hilo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 2.5. Watoto wanaoishi hapo walijaribu kupiga video kuonyesha maisha yao ya kila siku katika kipindi cha kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

    Hii ni sauti ya matangazo ya kituo cha TV cha Shine Kibera ambacho ni kituo kinachowashirikisha watoto wa makazi hayo. Ukiondoa mtayarishaji Job Moturi, waandishi wa habari, wapiga picha za video na watangazaji wote ni watoto wa hapa.

    "Mimi naitwa Sylvia Adhiambo, nina umri wa miaka 13. Mimi ni mwanahabari mwanafunzi."

    Tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi hivyo, makazi hayo yenye watu wengi yamefuatiliwa zaidi. Adhiambo na marafiki zake wanatumia kamera na kipaza sauti kurekodi maisha ya hapa.

    "Tangu kutokea kwa mlipuko wa COVID-19, tuliendelea kupiga picha ya video kuhusu maisha ya makazi wa Kibera. Ingawa familia mbalimbali wanaishi kwa pamoja, lakini wanakabiliana na changamoto tofauti."

    Mpiga picha ya video mwenye umri wa miaka 17, Irene Janet amesema, anatarajia kuwajulisha watu wote hadithi ya maisha ya Kibera. Tangu mlipuko huo kutokea, watu wengi wamepoteza ajira, na maisha yamekuwa magumu. Lakini anatarajia watu wa nje sio tu wataona hadithi mbaya za hapo, bali pia kujua jinsi watu hao wanavyopambana na virusi hivyo kwa hamasa.

    "Ni muhimu kurekodi hadithi hizo. Kwa sababu, tuliionesha dunia upande wa kuhamasika kwetu na kuwaelewesha kuwa hapa si tu kuna habari mbaya. Kama vile, watu wa Kibera wamejenga vituo vya kusafisha mikono. Unaweza kunawa mikono yako kila wakati. Hili ni jambo zuri walilofanya."

    Akiwa mtayarishaji wa vipindi katika kituo hicho cha TV, Bw. Moturi amesema, mradi huo ulianzisha mwaka 2013. Watoto wa makazi duni si tu wanahitaji misaada ya fedha, bali pia ni lazima kuwajengea uwezo wa kujiamini. Video zilizotengenezwa na watoto hao zimeoneshwa kwenye mtandao na kituo cha TV cha Kenya, na kuwapa watoto hao imani na kuwasaidia kupata ufundi.

    "Watoto hao wa kituo chetu, wanapenda kuonyesha hadithi za maisha ya Kibera, kwa sababu hapa kuna familia zao. Hivyo ina maana kubwa kuwajulisha watu wa nje hali ya makazi hayo. Tusiporipoti hadithi zao, watasahaulika. Watoto hao wametoa mchango mkubwa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako