• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatishia kujibu vikali hatua na kauli za Marekani zinazoingilia maslahi yake

    (GMT+08:00) 2020-06-01 19:18:25

    China imesema italinda kithabiti usalama wa mamlaka yake na maslahi ya kimaendeleo, na hatua na kauli zozote zinazoharibu maslahi ya China zitajibiwa vikali.

    Akizungumzia shutuma zisizo na msingi zilizotolewa na rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya China juu ya masuala mbalimbali ikiwemo utungaji sheria ya kulinda usalama wa taifa kwa Hong Kong, virusi vya Corona na masuala ya kibiashara, kutangaza kuzindua utaratibu wa kufuta kuipa Hong Kong hadhi maalum, na kuchunguza kampuni za China kuuza hisa zake katika masoko ya Marekani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema, Hong Kong ni ardhi ya China, na masuala yake ni mambo ya ndani ya China. Amesema Bunge la Umma la China kuamua kuanzisha na kuboresha mfumo wa kisheria na taratibu za utekelezaji wake ili kulinda usalama wa taifa katika Hong Kong ni kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba, kuhakikisha sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" inatekelezwa ipasavyo na kwa muda mrefu na kulinda utulivu na maendeleo ya muda mrefu ya Hong Kong, na nchi za nje hazina haki ya kuingilia kati.

    Zhao pia amesema, msingi wa ushirikiano wa kibiashara na kielimu kati ya China na Marekani ni kusaidiana na kunufaishana, lakini kwa muda mrefu, Marekani imetumia vibaya usalama wa taifa na kuzikandamiza kampuni za China, na sasa inatishia kuchunguza kampuni za China zinazouza hisa zake katika masoko ya Marekani na kuwawekea vikwazo vya visa wanafunzi wa China wanaosomea Marekani, hatua zinazokwenda kinyume cha kanuni ya ushindani wa soko na mawasiliano ya kirafiki kati ya watu wa China na Marekani.

    Kuhusu virusi vya Corona, Zhao amesema, virusi hivyo ni adui wa binadamu wote, na Marekani kuishutumu China na Shirika la Afya Duniani WHO ni kuhamisha ufuatiliaji wa watu wa Marekani na kuficha ukweli wa kushindwa kwake katika kudhibiti virusi hivyo, hatua ambayo sio ya maadili na haitaweza kudanganya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako