• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yachukua vigezo tofauti kwa maandamano yanayotokea nchini humo na mkoani Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-06-01 20:57:40

    Hivi karibuni mwanaume Mmarekani mwenye asili ya Afrika wa jimbo la Minnesota, Marekani, aliuawa na polisi wazungu, na tukio hili limesababisha maandamano makubwa katika miji zaidi ya 70 nchini humo. Serikali ya Marekani imedai maandamano hayo ni vurugu, na waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi ni wahalifu, na kuwasifu polisi waliogonga waandamanaji kwa gari na kusema ni mfano wa kuigwa. Pia imetishia kutuma majeshi na kuwafyatua risasi za moto waandamanaji. Shirika Kuu la Utangazaji la China limetoa tahariri, ikisema Marekani imechukua vigezo tofauti kwa maandamano yanayotokea nchini humo na mkoani Hong Kong.

    Tahariri hiyo inasema, huenda wanasiasa wa Marekani wamesahau kauli yao kuhusu maandamano yanayotokea mkoani Hong Kong, kwani walisema maandamano hayo ni "mandhari nzuri" ya Hong Kong, na wahalifu walioshambulia watu na kuteketeza majengo ni "watu wanaopigania demokrasia". Pia wamepaka matope polisi wa Hong Kong waliojitahidi kulinda utaratibu wa kijamii kwa kufuata sheria.

    Vyombo vya habari vya Hong Kong vilitoa ripoti ikisema, kuanzia mwaka 1995 hadi mwanzoni mwa mwaka 2015, Mfuko wa Demokrasia wa Taifa wa Marekani ulioanzishwa na bunge la nchi hiyo ulikuwa umetenga dola milioni 3.95 za Kimarekani kwa wapinzani wa mkoa wa Hong Kong. Tangu kutokea kwa maandamano mwaka jana kutokana na marekebisho ya sheria, mfuko huo umeshirikiana na wapinzani ili kufanya "mapinduzi ya kirangi". Zaidi ya hayo, wanasiasa wa Marekani akiwemo makamu wa rais Mike Pence, waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo, na spika wa baraza la seneta Nancy Pelosi kwa nyakati tofauti walikutana na wajumbe wa wapinzani wanaochochea vurugu mkoani Hong Kong, ili kuwaunga mkono.

    Kwa bahati mbaya, maandamano yanayotokea nchini Marekani yameitambulisha dunia kuwa, nchi hiyo ina vigezo tofauti kuhusu maandamano yanayotokea nchini humo, na katika nchi nyingine.

    Msomi maarufu wa Uingereza John Ross kwenye mtandao wa kijamii amesema, ikilinganishwa maandamano ya Marekani na Hong Kong, polisi wa Marekani wanawaua watu, na kukiuka haki za binadamu, tofauti na polisi wa Hong Kong. Hii inaonesha kuwa, kitu kinachojaliwa na wanasiasa wa Marekani si maslahi ya watu wa Hong Kong, bali ni maslahi yao ya kisiasa, na fursa ya kuizuia China kujiendeleza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako