• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: FA kuruhusu mashabiki 20,000 kuingia Wembley kutazama Fainali ya FA Cup

    (GMT+08:00) 2020-06-02 08:32:18

    Chama cha soka England FA kitaruhusu mashabiki 20,000 kuingia Wembley kutazama mchezo wa Fainali ya FA Cup Agosti 1 2020 endapo maambukizi ya virusi vya Corona yatakuwa yamepungua kwa kiasi kikubwa. Uwanja wa Wembley unachukua mashabiki 90,000 lakini wataingia mashabiki 20,000 kwa maana ya mashabiki 10,000 kwa kila timu sababu ya kukwepa mlundikano wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona.

    Wakati huohuo vilabu vya Ligi Kuu England vitaamua Alhamisi hii kama wameridhia matangazo ya mechi zao za LIVE kuwekwa sauti za mashabiki kutoka katika mechi ya FIFA 20 sababu ya EPL kuendelea bila mashabiki kutokana na Corona. Vituo mbalimbali vyenye haki ya kurusha matangazo ya LIVE ya mechi za Ligi husika, wanapambana kuhakikisha wanapata njia ya kuonesha mechi hizo zikiwa hazina mashabiki na kuendelea kuwa na mvuto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako