• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yarefusha tena muda wa marufuku ya kutoka nje usiku katika jimbo la Khartoum

    (GMT+08:00) 2020-06-02 09:09:53

    Kamati ya mambo ya dharura ya afya ya Sudan imetangaza kurefusha muda wa marufuku ya kutoka nje wakati wa usiku kwa wiki mbili zaidi katika jimbo la Khartoum kuanzia tarehe 3 mwezi huu, ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.

    Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw. Siddiq Tawer amesema muda wa marufuku ya kusafiri mjini Khartoum na majimbo mengine pia umerefushwa. Wakati huohuo, serikali itaondoa baadhi ya marufuku ya kutoka nje usiku, amabyo wananchi wanaruhusiwa kwenda nje kuanzia saa kumi na mbili alfajiri hadi saa tisa mchana.

    Jana jumatatu Wizara ya afya ya Sudan imethibitisha maambukizi mapya 147, na 113 kati ya hayo yametokea katika jimbo la Khartoum.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako