• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maambukizi ya COVID-19 nchini Nigeria hayajafika kilele

    (GMT+08:00) 2020-06-02 19:14:10

    Serikali ya Nigeria imeeleza wasiwasi wake kutokana na kuongezeka kwa kesi za virusi vya Corona nchini humo na kusema, kilele cha maambukizi ya ugonjwa huo bado hakijafika.

    Kituo cha Kukinga Magonjwa cha Nigeria (NCDC) jana, kiliripoti kesi 416 mpya za COVID-19 ambapo idadi ya ujumla ya kesi za ugonjwa huo imefikia 10,578, vifo 299 na watu 3122 wamepona. Pia imesema, watu wengi waliofariki kutokana na COVID-19 walikuwa na magonjwa mengine.

    Mwenyekiti wa tume maalum ya kupambana na COVID-19 nchini humo Bw. Boss Mustapha amesema, ni lazima kuwakumbusha watu kuwa kilele cha maambukizi bado hakijafika, na kwamba mapambano dhidi ya ugonjwa huo ni ya muda mrefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako