• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama tawala nchini Afrika Kusini chalaani ubaguzi wa rangi nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2020-06-02 20:08:04

    Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimelaani kuibuka kwa ubaguzi wa rangi nchini Marekani, na kutoa wito wa kutafuta suluhisho mwafaka la mvutano wa ubaguzi unaoendelea sasa.

    Taarifa ya Chama hicho iliyolifikia Shirika la Habari la China Xinhua imesema, wakati hatua zilizochukuliwa na mamlaka nchini Marekani katika kutoa hukumu kwa mmoja wa askari polisi alionekana kwenye picha akimkandamiza shingoni kwa goti lake Mmarekani mweusi George Floyd, inatia mashaka kuwa matukio ya polisi kutumia mabavu dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika yanaongezeka.

    Taarifa imesema, kesi za karibuni zinazohusu askari polisi kutumia nguvu dhidi ya Wamarekani weusi yameongeza ufuatiliaji usiokwepeka kuwa jamii ya Marekani imeshusha thamani ya maisha ya Wamarekani weusi. Chama hicho kimesema ANC ilipambana na kushinda ubaguzi wa rangi, na chama hicho hakitakaa kimya mbele ya mauaji ya watu weusi popote yanapojitokeza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako