• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakazi wa jiji la Nairobi nchini Kenya waandamana mbele ya ubalozi wa Marekani nchini humo kulaani mauaji ya George Floyd

    (GMT+08:00) 2020-06-02 21:09:09

    Zaidi ya watu 40 kutoka Kenya na nchi nyingine wameandamana mbele ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya, wakilaani mauaji ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd yaliyotokea nchini Marekani.

    Watu hao walikuwa na mabango yaliyokuwa na maneno kadhaa ikiwemo "Kumaliza Wazungu kwanza", "Maisha ya Watu weusi yastahili kujaliwa", na "Kukaa kimya ni kuunga mkono mabavu", ili kuomboleza kifo cha Floyd aliyeuawa na polisi wa kizungu, kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani, na vitendo vya kimabavu vya polisi nchini Marekani na Kenya.

    Awali, ubalozi wa Marekani nchini Kenya kupitia mtandao wa kijamii ulisema wizara ya sheria ya Marekani inafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo, kauli ambayo haikuwaridhisha Wakenya, ambao waliuliza baada ya raia weusi wa Marekani kuteswa na mfumo wa utumwa, ubaguzi wa rangi na mauaji kwa miaka 500, ni lini Marekani itaacha kusema inafanya uchunguzi, na kuchukua hatua halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako