• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: RB Salzburg watwaa ubingwa bila shamrashamra

    (GMT+08:00) 2020-06-03 08:38:24

    RB Salzburg waliwagaragaza Austria Lutenau kwa 5-0 na kutwaa ubingwa wa OFB Austrian Cup katika ushindi ambao kikawaida, ungelishuhudia mbwembwe na mihemko ya kila aina miongoni mwa wachezaji na mashabiki wa wafalme wa taji hilo. Hata hivyo, wakati ambapo soka imerejewa chini ya masharti makali katika juhudi za kudhibiti maambukizi zaidi ya ugonjwa wa Covid-19, ushindi wa Salzburg haukushuhudiwa na mashabiki uwanjani wala tukio la mashabiki kujitoma vichochoroni kusherehekea mafanikio ya kikosi chao. Licha ya wachezaji kukabiliana kwa karibu sana uwanjani kwa dakika 90 na hata wakati fulani kushikana wakiwania mipira ya kona, mipango kabambe iliwekwa kuhakikisha kwamba wanasoka wa Salzburg hawakaribiani sana walipokuwa wakifurahia ufalme wao baada ya kutawazwa mabingwa. Kikosi hicho cha kocha Jesse Marsch kililazimika kusimama kwenye zulia kubwa lililokuwa na michoro ya maumbo ya mviringo yaliyobainisha mahali ambapo kila mchezaji alistahili kusimamia ili kudumisha umbali wa hadi mita moja kati yao. Nahodha Andreas Ulmer alinyanyua kombe katika uwanja mtupu wa Worthersee bila mashabiki. Mtindo wa kusherehekea ubingwa kwa namna hiyo huenda sasa ukaigwa na vikosi vyote barani Ulaya hasa ikizingatiwa kuwa mapambano mengi yaliyosimamishwa yanarejea Juni 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako