• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yahitaji pato la taifa liongezeke kwa zaidi ya asilimia 5 ili kufufua sekta ya biashara

    (GMT+08:00) 2020-06-03 10:07:36

    Jumuiya ya kibiashara ya Afrika Kusini imesema serikali ya Afrika Kusini inahitaji pato la taifa liongezeke kwa zaidi ya asilimia 5, na kufanya marekebisho juu ya muundo wa kiuchumi, ili kufufua uchumi wa nchi baada ya kukumbwa na janga la virusi vya Corona.

    Ofisa mkuu mtendaji wa jumuiya hiyo Bw. Cas Coovadia amesema Afrika Kusini iko kwenye changamoto ya kiuchumi, kwa kuwa tayari ilikumbwa na msukosuko wa kifedha na kudidimia kwa uchumi kabla ya virusi vya Corona kutokea.

    Ameongeza kuwa inapaswa kufanya pato la taifa liongezeke kwa zaidi ya asilimia 5, na kujenga muundo wa kiuchumi wenye ushirikishi na usawa, hali ambayo inawataka wadau wote watoe kipaumbele kwa maslahi ya nchi. Zaidi ya hayo makampuni na serikali zinatakiwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na wa nje, na kuyafanya makampuni yawe mwenzi wa kuaminika, ili kusaidia nchi hiyo kuondokana na msukosuko huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako