Chelsea jana imefuata nyayo za Liverpool kuwa miongoni mwa klabu zinazotoka Premier League kupiga goti moja kama ishara ya kuunga mkono harakati za 'Black Lives Matter' kupinga ubaguzi wa rangi kufuatua kifo cha Mmarekani mwenye asili ya watu weusi, George Floyd. Wachezaji kutoka katika klabu ya jiji la London wamepiga magoti wakati wa mazoezi katika viwanja vya Cobham. Mlindalango, Kepa ameelezea katika akaunti yake ya twitter kwa kuandika ujumbe kuwa inatosha, "Inatosha, sisi sote ni binadamu. Pamoja tupo imara." Wachezaji wa klabu ya Newcastle nao walipiga magoti katika kuunga mkono harakati za ubaguzi. Jumatatu kikosi cha Liverpool kilipiga magoti kwa kuonyesha ishara ya umoja juu ya kifo cha Mmarekani mweusi aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi kabla ya kuanza mazoezi yake katika uwanja wa Anfield.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |