• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Matumizi ya intaneti yaongezeka

    (GMT+08:00) 2020-06-03 18:42:33

    Watumiaji wa vivurushi vya data kupitia kwa rununu nchini Uganda wameongezeka kutoka milioni 15.4 mwezi oktoba mwaka 2019 hadi milioni 16.9 Desemba 2019.

    Tume ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) imesema kwenye ripoti yake ya kila mwaka kuwa kumekuwa pia na ukuaji wa kuvutia katikahuduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu na mtandao kwa robo ya mwisho ya 2019.

    Usajili wa simu za rununu nchini Uganda umefikia milioni 26.7 mnamo Desemba 2019, asilimia 3 kutoka kwa usajili wa Septemba 2019.

    Ripoti ya robo mwaka, ambayo inategemea uwasilishaji wa leseni, inaonyesha jumla ya nyongeza ya milioni 1.9 kwenye mtandao wa simu katika robo nne zilizopita.

    Kulingana na ripoti hiyo, huduma za kifedha za simu ziliendelea kupata ukuaji endelevu. Karibu akaunti mpya za pesa 700,000 zilisajiliwa katika robo ya mwisho ya Desemba 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako