• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cristiano Ronaldo ampiku Lionel Messi kwa kupokea mkwanja mrefu

    (GMT+08:00) 2020-06-04 09:00:32

    Cristiano Ronaldo amempiku nyota mwenzake, Lionel Messi kwenye mchakato wa wanasoka waliovuna pesa nyingi zaidi kwa mwaka 2020 kama inavyofichua orodha mpya ya jarida la Forbes. Mjumuiko wa mishahara yake pamoja na pesa nyingine anazovuna kupitia soka yake uwanjani pamoja na dili za matangazo umemshuhudia Ronaldo akiweka kibindoni Pauni milioni 85.8 kwa mwaka 2020, akiwa amezidiwa na nyota wa tenisi, Roger Federer, ambaye anashika usukani kwa kuwa mwanamichezo aliyevuna pesa nyingi zaidi duniani. Messi anashika namba tatu kwenye orodha yote, lakini ni namba mbili kwa wanasoka, kutokana na kuvuna Pauni milioni 83.4, huku hilo likija baada ya Barcelona kuamua kumpunguzia mshahara wake kutokana na janga la corona. Anayefuatia kwenye orodha hii ni Mbrazili, Neymar ambaye amevuna Pauni milioni 76.6, huku nyota huyo wa Paris SaintGermain, akivuna Pauni milioni 20 kutoka kwenye dili zake za matangazo. Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah anafuatia kwenye orodha hiyo, lakini akishika namba moja kwa upande wa Ligi Kuu England baada ya kuvuna Pauni milioni 28.2 ndani ya mwaka huu na kumpiku straika namba moja wa Ufaransa, Kylian Mbappe. Mbappe amevuna Pauni milioni 27.1 ndani ya mwaka huu, huku orodha hiyo ikiwahusu pia mastaa Andres Iniesta, anayekipiga Vissel Kobe ya Japan, kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil, nyota wa Manchester United, Paul Pogba, kiungo wa Shanghai SIPG, Oscar na mkali wa Barcelona, Antoine Griezmann.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako