• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Hassan Mwakinyo aweka mipango kabambe ya kupigana

    (GMT+08:00) 2020-06-04 09:02:00

    Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kufuatia kuporomoka kwenye viwango vya ngumi duniani, Hassan Mwakinyo ameeleza mipango yake mipya. Mwakinyo bondia namba moja nchini Tanzania kwenye uzani wa super welter aliporomoka hadi nafasi ya 76 kwenye viwango vya ngumi duniani miezi kadhaa iliyopita kutoka nafasi ya 21. Mwakinyo alisema bado ana ndoto ya kuwa bondia namba moja wa dunia na mikakati yake ni kucheza mapambano matano mfululizo ambayo atayashinda kwa knock out (KO) kipindi hiki. Bondia huyo ambaye sasa ana nyota mbili na nusu kutoka nne za awali alisema promota wake, Ally Mwanzoa ameshaanza mchakato wa yeye kurudi ulingoni licha ya pambano lake lililokuwa lipigwe Ujerumani kuondoshwa kucheza. Katika pambano hilo ambalo liliahirishwa kutokana na tahadhari ya virusi vya corona, Mwakinyo angezichapa na Jack Culcay ambaye sasa atacheza na bondia mwingine baada ya Mwakinyo kuporomoka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako