• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema bandari kavu Mai Mahiu kupunguza maambukizo ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-04 10:10:35
    Kenya imesema bandari kavu Mai Mahiu iliyojengwa na kufadhiliwa na China itasaidia pakubwa katika kupunguza maambukizo ya virusi vya Corona katika eneo zima la Afrika mashariki.

    Akizungumza na Radio China kimataifa baada ya kuzuru bandari hiyo kavu, waziri wa uchukuzi wa Kenya Bw James Macharia amesema Kenya inalenga kufanya mazungumzo na nchi jirani ambazo zinatumia bandari ya Mombasa kusafirisha mizigo yao umuhimu wa bandari hiyo kavu katika kupunguza maambukizo ambayo yamekuwa yakiongezeka katika nchi za Afrika mashariki. Amesema maambukizo mengi yamekuwa yakitokea katika maeneo ya mpakani lakini hivi sasa tayari wamefanya mazungumzo jirani zao na kukubaliana kuwekeza zaidi kwa magari yenye maabara ili kuwafanyia watu vipimo na hatimaye kufanya makubaliano ya pamoja kwa matokeo ya vipimo.

    "Kulikuwa na hatari ya juu sana kumruhusu mtu kuingia nchini eti kwasababu amefanyanyiwa vipimo. Ni kutokana na hilo ambapo tukafanya makubaliano na ndugu zetu jirani ya kufanya vipimo katika sehemu zote mbili mpakani. Pia tulikubaliana kuwa kila upande utawekeza zaidi kwa magari yenye maabara kwa hiyo hilo tatizo tayari tumesuluhisha".

    Bandari hiyo ambayo imejenga kwa gharama ya shilingi bilioni 6.5 inakamilika wakati ambapo madereva wengi wa malori ya mizigo wamekuwa wakikwama mpakani kufuatia hofu ya maambukizo ya virusi vya Corona. Madereva hao wameitaka serikali kutafuta njia ya kudumu itakayosaidia kutokomeza kabisa matatizo wanayokumbana nayo haswa wakati huu wa kuenea kwa virusi vya Corona. Paul ni miongoni mwa madereva hao wa Malori

    Hata hivyo waziri Macharia amewataka madereva wa Malori wasiwe na wasiwasi kwa kuwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja watakuwa wamekarabati reli ya zamani itakayounganishwa na ya kisasa itakayotoka Mahi Mahiu hadi Malaba ili kuwaokoa kutoka kwa tatizo wanalopata hivi sasa.

    "Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tutakuwa tumekarabati reli ya za zamani na kuinganisha ya sasa kutoka Mahi Mahiu. Reli hiyo itakwenda hadi kituo cha Longonot na hadi mpakani Malaba.Huu ndio mtandao wa reli ambao tunaunda kutoka Bandari ya Mombasa hadi malaba.Hii ndio njia pekee ya kusuluhisha hili tatizo na pia kuzuia kutokea kwa tatizo katika siku za usoni ambapo unaona malori yamepanga folebi ya karibu kilomita 60.Huu mtandao wa reli ndio utakaokuwa ni suluhisho kwa hili tatizo".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako