• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani itapata hasara kubwa kama ikitengana na China

    (GMT+08:00) 2020-06-05 17:13:54

    Gazeti la the Wall Street Journal la Marekani hivi karibuni limetoa makala, ikiuliza kama Marekani iko tayari kupata hasara kubwa kwa kutengana na China. Makala hiyo inaonya kuwa wanasiasa wenye msimamo mkali dhidi ya China wanapaswa kutambua hasara kubwa zitakazotokea kutokana na Marekani na China kutengana katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara na elimu.

    Makala hiyo imechapishwa wakati baadhi ya wanasiasa wa Marekani wakitetea kwa nguvu maoni ya kutenganisha uchumi wa nchi hiyo na China, na kuondoa ushawishi wa China katika mnyororo wa bidhaa. Kwa mfano mshauri wa uchumi wa Ikulu ya Marekani Lawrence Kudlow hivi karibuni amehimiza tena makampuni ya nchi hiyo yaliyoko China kurudi nyumbani.

    Hata hivyo, kwa maoni ya wanauchumi wenye busara, makampuni ya Marekani kurudi nchini humo kutoka China ni ndoto ya wanasiasa wa Marekani, kwani makampuni ya kuvuka mipaka hupanga uzalishaji wao kwa kufuata utaratibu wa kisoko, ili kupata faida zaidi. Makampuni ya Marekani yakijitenga na China, yatakosa soko kubwa mno la nchi hiyo yenye watu bilioni 1.4. Licha ya hayo, katika miongo mitano iliyopita, Marekani imegeuka kuwa nchi ambayo uchumi wake unategemea zaidi sekta za fedha na huduma kutoka nchi yenye nguvu kubwa ya kiviwanda, na imekosa rasilimali ya kutosha ya uzalishaji wa kiviwanda. Kama ikirudisha makampuni yake ya uzalishaji kutoka China, itakuwa vigumu kwake kupata nguvukazi ya kutosha.

    Ukweli ni kwamba makampuni mengi ya Marekani yamekwenda kinyume na matumaini ya wanasiasa wa nchi hiyo. Hivi karibuni, Kampuni ya Honeywell ya Marekani imezindua makao makuu yake ya nchi zinazoibuka kiuchumi katika mji wa Wuhan, China, Kampuni ya Tesla imeongeza uwezo wa uzalishaji mjini Shanghai, Kampuni ya Exxon Mobil imezindua mradi wake mkubwa wa kemikali mkoani Guangdong, na Kampuni ya Starbucks imetangaza kujenga eneo la kiuvumbuzi la kahawa nchini China.

    Gazeti la the Wall Street Journal kwenye makala yake limesema, soko kubwa la China haliwezi kupuuzwa, na hii ni hali halisi, na pia ni maoni ya pamoja ya dunia nzima. Kauli ya wanasiasa wa Marekani ya kutenganisha uchumi wa nchi hiyo na China ni ndoto, na haiwezi kubadilisha nia ya makampuni ya kuvuka mipaka yakiwemo makampuni ya Marekani ya kujiendeleza nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako