• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari vya Marekani vyasema rais wa nchi hiyo ametengwa na washirika wake

    (GMT+08:00) 2020-06-05 17:16:43

    Washirika wa Marekani katika bara la Ulaya hawana tena imani kuwa rais Donald Trump wa nchi hiyo anaweza kuwa msaada kwao, ikiwa ni baada ya miaka kadhaa ya vitendo vya upande mmoja vya Marekani.

    Makala iliyochapishwa jumanne katika gazeti la New York Times ilisema, mapema wiki hii, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliamua kutohudhuria mkutano wa Nchi Saba (G7) ambao awali ulipangwa kufanyika katika Ikulu ya Marekani baadaye mwezi huu. Kansela huyo alitoa sababu ya kutohudhuria kuwa ni janga la virusi vya Corona, lakini ofisa wa ngazi ya juu wa Ujerumani amesema sababu halisi ni kwamba Bi. Merkel anaamini kuwa maandalizi kamili ya kidiplomasia hayajafanywa, na pia hakutaka kuonyeshwa kama anaipinga China. Lakini pia ofisa huyo amesema, Bi. Merkel anapinga mpango wa rais Trump wa kumwalika rais wa Russia, Vladmir Putin, na hakutaka kuonekana kuwa anaingilia kati siasa za ndani za Marekani.

    Vilevile, Makala hiyo imesema, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaamini kuwa rais Trump amevuruga usalama wa Ulaya kupitia kitendo chake cha upande mmoja cha kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran na karibu makubaliano yote ya kudhibiti silaha kati yake na Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako