• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaeleza kuunga mkono nafasi ya WHO katika utafiti wa chanjo

    (GMT+08:00) 2020-06-05 18:59:07

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema China inaunga mkono nafasi muhimu ya Shirika la Afya Duniani WHO katika kuratibu tafiti za chanjo dhidi ya virusi vya Corona, na kuahidi kuendelea kuchangia ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na virusi hivyo na maendeleo husika ya kimatibabu.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang alishiriki kwenye mkutano wa kilele wa chanjo duniani uliofanyika jana kwa njia ya video ukiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa Muungano wa Kimataifa kwa Chanjo na Kinga Mwili GAVI, na kuhudhuriwa na viongozi kutoka nchi zaidi ya 30 na wakuu wa mashirika ya kimataifa.

    Geng amesema chanjo ni ngao yenye nguvu zaidi katika kushinda virusi hivyo, na China itaendelea kuunga mkono ushirikiano wa kimataifa na maendeleo ya chanjo, na pia kuendelea kutoa mchango kwa ajili ya kuhakikisha chanjo zinapatikana na kumudika katika nchi zinazoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako