• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapongeza Bw. Endaishmiya kuwa rais mpya wa Burundi

    (GMT+08:00) 2020-06-05 19:05:39

    China imepongeza Bw. Evariste Endaishmiya kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Burundi, na kusema iko tayari kushirikiana na Burundi kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili upande ngazi ya juu zaidi.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inaamini kuwa, chini ya uongozi wa rais Endaishmiya, serikali na watu wa Burundi watapata mafanikio makubwa zaidi katika maendeleo ya nchi. Amesema China inapenda kushirikiana na Burundi kuimarisha uaminifu wa kirafiki, kuongeza ushirikiano wa kunufaishana na kuzidisha uratibu wa kimataifa.

    Habari zinasema, mahakama ya katiba ya Burundi jana imetangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais, ambapo mgombea kutoka chama tawala cha Burundi Evariste Endaishmiya ameshinda katika uchaguzi huo na kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Burundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako