• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Meya wa Washington D.C aipa jina barabara kwa heshima ya waandamanaji wanaotaka usawa kwa Wamarekani weusi

    (GMT+08:00) 2020-06-06 17:54:20

    Meya wa Washington D.C Muriel Bowser jana aliipa jina sehemu ya barabara iendayo ikulu ya White House ya Marekani "Black Lives Matter Plaza," ikiwa na maana "Barabara ya Maisha ya Watu Weusi ni Muhimu", kwa ajili ya kuwaheshimu waandamanaji wanaondamana kwa siku kadhaa sasa katika mji mkuu huo wakitaka kuwepo usawa wa rangi.

    Wafanyakazi walifanya kazi usiku kucha kuchora kauli mbiu hiyo kwa herufi kubwa za rangi ya njano na baadaye kutundikwa kwenye kona za barabara za 16th na H, eneo ambalo lipo kanisa la St. John's Episcopal. Rais Donald Trump Jumatatu alipiga picha katika kanisa hilo la kihisoria, na kusababisha utata huku askari wakiripotiwa kutumia silaha zisizoangamiza kutawanya waandamaji walio karibu ili kumpisha rais na msafara wake. Ijumaa Bowser alimtumia barua Trump na kumnasihi kuondoa askari wote kwenye mji wake baada ya kuamuru askari kuwaondoa kwa nguvu waandamanaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako