• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka kuhusu mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-07 17:21:39

    Ofisi ya habari ya baraza la mawaziri la China leo asubuhi (June 7) imetoa waraka kuhusu mapambano dhidi ya virusi vya Corona wenye jina "Mapambano dhidi ya COVID-19: Juhudi za China".

    Waraka huu umetolewa wakati China kimsingi imefanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona ya ndani na yale kutoka nje. Waraka huo wenye sura nne, unaeleza juhudi za China kwenye kazi ya kinga, udhibiti na kutoa matibabu kwa wale walioambukizwa, na kusema kiwango cha utoaji wa matibabu na kupona kwa waliombukizwa kimefikia asilimia 94.

    Ugonjwa huu ulioanza kuenea nchini China mwezi Januari ulisimamisha shughuli zote za kiuchumi na kijamii hapa China, na kuzifanya mamlaka nchini China kupambana na ugonjwa huo kwa njia zote, huku zikizingatia namna ya kupunguza madhara yake kwenye mambo ya uchumi sio kwa China tu, bali kwenye kwa nchi nyingine duniani.

    Moja ya mambo yanayotia moyo kwenye waraka huo, ni msimamo wa China kuhusu ushirikiano wa kimataifa kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona. Waraka umesema dunia "itaibuka kutoka kwenye hali ngumu katika historia ya binadamu na kuingia kwenye kipindi kizuri zaidi". Lakini hili linaweza kufanikishwa kama nchi zote zitashirikiana na kuwa na mwitikio wa pamoja.

    Waraka huo pia umekumbusha kuhusu umuhimu wa sayansi na teknolojia kwenye mapambano dhidi ya COVID-19, nyenzo ambazo zimetumiwa vizuri na China kwenye kufanikisha mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Kwa sasa hali nchini China kimsingi iko shwari, karibu shughuli nyingi za kiuchumi zimerudi katika hali ya kawaida na uzalishaji unaendelea. Hata hivyo tahadhari bado inaendelea kuwepo, kama vile upimaji wa joto kila watu wanapoingia kwenye majengo ya umma na makazi, uvaaji wa barakoa na hata kudumisha umbali kati ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako