• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la matumizi lazinduliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2020-06-07 19:05:03

    Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na serikali ya Beijing wamezindua tamasha la matumizi jijini Beijing, likilenga kuchangia juhudi za kufufua na kustawisha shughuli za biashara kwenye masoko na maduka mbalimbali. Imefahamika kuwa katika tamasha hilo litakaloendelea hadi mwishoni mwa mwaka huu, serikali ya Beijing itatoa kuponi zenye thamani ya Yuan bilioni 12.2, sawa na dola bilioni 1.7 za kimarekani, kutangaza sera mfululizo za kuhimiza matumizi ya aina mpya, na kuandaa shughuli husika takriban 400, zikiwemo mauzo ya bidhaa zinazotoka mkoa wa Hubei, ulioathirika vibaya zaidi na janga la corona, kupitia matangazo ya moja kwa moja mtandaoni.

    CMG likiwa ni shirika la habari lenye nguvu zaidi nchini China, itachangia kutangaza na kuuza bidhaa kupitia vyombo vyake mbalimbali. Inakadiriwa kuwa jana bidhaa zenye thamani ya Yuan bilioni 1.4, sawa na dola za kimarekani milioni 200 ziliuzwa ndani ya saa 3 kupitia CMG.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako