• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CORONA: Jadon Sancho wa Borussia Dortmund apigwa faini kwa kukiuka kanuni za kuvaa barakoa

    (GMT+08:00) 2020-06-08 09:15:08

    Chipukizi Jadon Sancho wa klabu ya Borussia Dortmund amepigwa faini na vinara wa soka ya Ujerumani baada ya kuonekana akinyolewa bila ya kuvalia barakoa. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni mzawa wa Uingereza alionekana kwenye picha na mchezaji mwenzake, Manuel Akanji ambaye pia amepigwa faini. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wasimamizi wa Ligi Kuu ya Ujerumani (DFL), wawili hao walikuwa wamekiuka kanuni za kimsingi za afya na kujikinga kwao hakukufikia viwango inavyotakikana. Hata hivyo, Dortmund iliwatetea wanasoka hao vikali kwa kusisitiza kwamba hawakuwa wamevunja masharti yoyote kati ya sheria za afya zinazodhibiti soka ya Bundesliga. Gazeti la Bild nchini Ujerumani liliweka kwenye mtandao wa Twitter habari na picha zilizowaonyesha Sancho na Akanji wakiwa karibu sana wakati wa kunyolewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako