• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubaguzi wa rangi unaofanywa na polisi umekuwa maradhi sugu nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2020-06-08 10:35:16

    Jina la mtaa mmoja ulioko karibu na Ikulu ya Marekani Ijumaa lilibadilishwa kuwa"BlackLives Matter". Tangu Mmarekani mwenye asili ya Afrika George Floyd auawe na polisi mzungu mjini Minneapolis, watu wamefanya maombolezo kwa njia mbalimbali, na hata baadhi yao wamefanya maandamano makubwa ili kupinga ubaguzi wa rangi ambao umekuwa maradhi sugu ya kijamii nchini Marekani.

    Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Gazeti la the New York Times la Marekani, katika mji wa Minneapolis ambao watu wenye asili ya Afrika wanachukua chini ya asilimia 20, asilimia 60 ya watu waliowahi kutendewa kimabavu na polisi ni watu weusi. Takwimu zinaonesha kuwa uwezekano wa kukamatwa na polisi kwa watu weusi ni mara 5 hadi 8.7 ya wazungu mjini humo.

    Profesa Keith Mays wa Chuo Kikuu cha Minnesota anayeshughulikia utafiti wa mambo ya watu weusi na Afrika, amesema haki ya kijamii ya Marekani haijagawanywa kwa kila mtu kwa usawa, watu wenye asili ya Afrika hutendewa bila haki na usawa. Ameongeza kuwa kama hali hiyo itaendelea, Marekani haitaaminiwa tena na jumuiya ya kimataifa kwa nia yake ya kutetea haki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako