• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yasifu mafanikio ya China katika kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-08 18:53:34

    Jumuiya ya kimataifa imesifu waraka kuhusu mapambano dhidi ya virusi vya Corona uliotolewa na China, na kusema kuwa uzoefu wa China wa kupambana na janga hilo umeongoza dunia, na China imepata mafanikio makubwa katika mapambano hayo.

    Balozi wa zamani wa Pakistan nchini China Bw. Zamir Awan amesema, waraka huo ni muhimu na unaeleza mchakato wa China katika kupambana na janga la COVID-19, na takwimu husika ambazo pia ni mwongozo mzuri kwa dunia.

    Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa virusi vya binadamu cha chuo cha udaktari cha Maryland nchini Marekani Bw. Robert Gallo amesema, utafiti wa kisayansi wa China na matibabu ni mfano mzuri wa kuigwa, na hatua za karantini zilizochukuliwa na serikali ya China zimepata ufanisi.

    Waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Sudan Bw. Abdalla Hamdok anatarajia kuwa nchi hiyo itajifunza uzoefu wa China katika kuzuia, kudhibiti na kutibu virusi hivyo, ili kushinda mapambano hayo mapema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako