• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakazi ya Hong Kong waweza kutekeleza vizuri zaidi haki zao chini ya sheria ya usalama wa taifa

    (GMT+08:00) 2020-06-09 09:28:40

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, sheria mpya ya usalama wa taifa kwa Hong Kong itawasaidia wakazi wa Hong Kong kutekeleza vizuri zaidi uhuru na haki zao halali kwenye mazingira salama.

    Bibi Hua amesema msingi wa kisheria wa kutekeleza sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili" na kutunga sheria ya usalama wa taifa kwa mkoa wa Hong Kong ni Katiba ya China na Sheria ya Msingi, na wala sio Azimio la Pamoja la China na Uingereza.

    Bibi Hua pia amesema sheria mpya ya usalama wa taifa kwa Hongkong inalenga aina nne za vitendo, yaani kuifarakanisha nchi, kupindua utawala wa serikali kuu, kupanga na kutekeleza vitendo vya kigaidi, uingiliaji kutoka nje wa mambo ya Hong Kong na vitendo vya baadhi ya watu vya kuhujumu usalama wa taifa. Hivyo hakuna haja kwa wawekezaji kutoka nje na wakazi ya Hong Kong wanaofuata sheria kuwa na wasiwasi wowote.

    Habari zinasema, wakazi milioni 3 wa Hong Kong na makampuni ya nje kama vile HSBC, Jardine Matheson, Swire Group na Standard Chartered yameonesha uungaji mkono kwa utungaji wa sheria hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako