• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yapaswa kuheshimu mamlaka halali ya China ya kulinda usalama wa taifa mkoani Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-06-09 09:29:01

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ameeleza matumaini yake kuwa Uingereza itaheshimu mamlaka halali ya China kulinda usalama wa taifa katika mkoa wa Hong Kong kwenye mazungumzo yake kwa njia ya simu na mwenzake wa Uingereza Bw. Dominic Raab.

    Bw. Wang amesema mfumo wa upande mmoja utaharibu amani na utulivu wa kimkakati wa dunia. Amesema China na Uingereza zinabeba majukumu ya kutetea taratibu za pande nyingi na kulinda kwa pamoja mfumo wa kimataifa wenye Umoja wa Mataifa kuwa kiini chake, na utaratibu wa kimataifa ulioko kwenye msingi wa sheria za kimataifa.

    Pia amesema mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China ambayo China hairuhusu uingiliaji kutoka nje, na usalama wa Hong Kong unahusiana na maslahi makuu ya China.

    Bw. Raab amesema Uingereza inapenda kuendeleza uhusiano mzuri kati ya pande hizo mbili, na ana imani kuwa, nchi hizo mbili zitaongeza ushirikiano katika masuala makuu ya kimataifa na kikanda kama vile masuala ya mabadiliko ya tabianchi, na suala la nyuklia la Iran baada ya mlipuko wa COVID-19. Pia amesema, chini ya uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili, Uingereza inapenda kuendelea kubadilishana maoni na China kwa msingi wa kuheshimiana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako