• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mkwasa: Wachezaji hawana utimamu wa mwili

    (GMT+08:00) 2020-06-09 16:23:20

    Kocha msaidizi wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa amesema wachezaji wake hawana utimamu wa mwili (hawako fit), ukilinganisha na walivyoonekana wapinzani wao KMC FC, katika mchezo wa wa kirafiki uliopigwa jumapili Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Katika mchezo huo Young Africans walikubali kupoteza kwa kufungwa mabao matatu kwa sifuri, huku wakionyesha kiwango duni mbele ya mashabiki wao waliofika kwa wingi uwanjani hapo. Mkwasa amesema ni dhahiri walistahili kupoteza mchezo huo, kutokana na makosa mengi aliyoyaona kwa wachezaji wake, ambao walianza maandalizi ya kuendelea na ligi kuu, majuma mawili yaliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako