Kulingana na data kutoka idara za serikali biashara ya thamani ya takriban Sh200 milioni huendeshwa katika eneo hilo kila siku.
Baada ya tamko la rais, malori yameanza kuleta bidhaa za kuuza, huku wahudumu wa matatu na waendeshaji wa bodaboda wakirejelea hudumu za kuwasafirisha watu.
Eastleigh na Old Town Mombasa ni maeneo yaliyofungwa mwezi mmoja uliopita baada ya kuandikisha idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya virusi vya corona.
Hatua hiyo iliathiri uchumi wa Eastleigh; eneo ambalo ni la pili kwa ukubwa kibiashara Nairobi, baada ya Westlands.
Takwimu kutoka Shirika la Kitaifa la Takwimu (KNBS) zinaonyesha kuwa Eastleigh huchangia asilimia 25 ya jumla ya mapato ya Kaunti ya Nairobi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |