• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi afariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo

    (GMT+08:00) 2020-06-10 09:31:45

    Serikali ya Burundi imetoa taarifa kuwa rais wa nchi hiyo Bw. Pierre Nkurunziza amefariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo.

    Taarifa hiyo imesema rais Nkurunziza alianza kutojisikia vizuri tarehe 6, baada ya kuangalia mechi moja ya mpira wa wavu na kupelekwa hospitali mkoani Karusi. Hali yake ya afya iliboreka tarehe 7, lakini ilizorota ghalfa asubuhi ya tarehe 8. Alifariki dunia baada ya saa kadhaa za juhudi za kunusuru maisha yake kushindwa. Serikali imetangaza siku 7 za maombolezo ya taifa.

    Kwa mujibu wa katiba ya Burundi spika wa bunge la nchi hiyo Bw. Pascal Nyabenda atachukua majukumu ya rais na kuongoza serikali mpaka rais mteule Evariste Ndayishimiye atakapoapishwa mwezi Agosti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako